Posts

Ashindwa kulipa bili ya mpenzi wake hotelini

Image
  Mwanaume mmoja nchini Kenya anayefahamika kwa jina la Henry Ochola Midiwo anashtakiwa kwa kushindwa kulipa bili ya Ksh 7000 sawa na Tsh 140,838 kwa kuigiza chakula na pombe kali hotelini akiwa na mpenzi wake. Henry ameachiwa kwa dhamana ya Ksh 200,000 na kesi yake inatarajiwa kusikilizwa April 25 mwaka huu. Henry alifika hotelini akiwa na mwanamke ambaye aliagiza chakula na pombe kali kisha wakaelekea chumbani pamoja. Baada ya masaa kadhaa alipelekewa bili yake na hakuwa na uwezo wa kuilipa

Paul Makonda Afunguka "Nafahamu Kuna Mkakati Unaoratibiwa na Makundi 5 Kuangamiza Maisha Yangu"

Image
  Kutoka Page ya Instagram ya Paul Makonda: "Nafahamu kuna mkakati unaoratibiwa na Makundi 5 kuangamiza maisha yangu. 1) WAUZA MADAWA YA KULEVYA 2)WANUFAIKA NA MADAWA YA KULEVYA 3) MASHOGA 4)WANAOKESHA USIKU KUCHA KUTAFUTA KULIPA KISASI KWA WASAIDIZI WA DR MAGUFULI. 5) WALIOWAHI KUWA SEHEMU YA ……. Nafahamu pia juu ya mbinu zinazoandaliwa ili kuniuwa kwa faida ya familia zao pamoja na kutengeneza mashaidi wa uongo ili mnipe kesi ya uhujumu uchumi. Mambo mawili najiuliza 1)PAMOJA NA KAZI ZOTE NZURI NILIZOZIFANYA KWA CHAMA CHANGU,SERIKALI YANGU NA WANANCHI WA DAR HAYA NDIYO MALIPO YAKE? 2)Hakika ukiwa mtumishi mwaminifu unaetetea haki za wanyonge tena ukitokea kwenye familia masikini haya ndiyo malipo yake ? MTU aliejemga hospital , aliejenga ofc cha CCM, Magari ya police 👮‍♀️, ofc za Walimu, vituo vya police, shule za secondary mpaka na msingi, kutibu wagonjwa mpaka Meli kuja Tanzania,kuhudumia Makundi mbali mbali mpaka kuiunganisha Serikali na Viongozi wa Dini. leo hii naonekana e...

Kijana Afikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Kukata Viuno Hadharani

Image
  Maulid Hussein Abdallah, mkazi wa Kijiji cha Mwera Wilaya ya Magharibi Unguja visiwani Zanzibar, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukata viuno hadharani. Kijana huyo anatuhumiwa kutenda kosa hilo katika Mji wa Kibole, Wilaya ya Kati, Kusini Unguja majira ya saa 11 jioni ambapo inaelezwa kwamba akiwa amevalia mtandio, alianza kucheza kwa kukata viuno hadharani, jambo ambalo ni kosa la kisheria visiwani humo. Mshitakiwa huyo amepinga mashtaka hayo na kuiomba mahakama kumpa dhamana kwa kuwa yupo kituo cha polisi siku nyingi. Amri ya kupelekwa rumande imetolewa na Hakimu Safia Waziri, baada ya mshitakiwa kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya TZS 100,000 pamoja na barua zikiambatana na kopi ya kitambulisho cha Mzanzibar. Mshitakiwa baada ya kushindwa kutekeleza masharti hayo, mahakama iliamuru arudishwe mahabusu hadi Aprili 25, mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi.

Dar Mpya waonywa habari za Bunge

Image
  Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Mwansasu amevionya vyombo vya Habari na wahariri wa madawati ya Habari juu ya uandishi wa Habari zisizokuwa na ukweli hasa zinazohusu Bunge na wabunge wote. Akizungumza jana Bungeni Jijini Dodoma wakati akifunga Kikao cha sita, mkutano wa 7 bunge la 12, Dkt. Tulia amesema Waandishi wa Habari wamepewa ruhusa ya kuingia Bungeni na wamepewa nafasi ya kufanya mahojiano na mbunge yeyote ambae kuna jambo wanahitaji ufafanuzi hivyo hawapaswi kuandika mambo ya kutunga. Spika Dkt Tulia, amesema kuwa Bunge halihitaji kufanya kazi kwa ubaya na waandishi wa habari kwa kuwa wao wanawasaidia kutoa taarifa za mambo yayayotokea na kwa manufaa ya majimbo yao na hawataki ifike wakati ambao baadhi ya vyombo vitafungiwa kujihusisha na masuala ya Bunge kwa kukiuka kanuni. “Sasa tuko katika kipindi ambacho yatu wasituvute sana alafu wakaanza kuitwa hapa maana mamlaka hayo tunayo, Vyombo vya habari tupo tayari kuwapa ushirikiano na tut...

RAISI AMTEUA SOPHIA SIMBA

Image
  Rais Samia amteua Sophia Simba mwananclm. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT), Sophia Simba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jami (ISW). Tarifa iliyotolewa leo Jumatano Aprili 13, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus imesema kuwa uteuzi huo umeanza mara moja. Sophia Simba aliyezaliwa Julai 27, 1950, ni mwanasiasa wa kutoka CCM aliyeshika nyadhifa mbalimbali katika chama hicho na Serikalini. Kitaaluma ni mwanasheria aliyepata elimu yake katika chuo Kikuu cha Dar es Dar es Salaam na baadaye Chuo kikuu cha Zimbabwe.   Aliwahi kuwa diwani na baadaye akawa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) nafasi iliyomwezesha kuwa Mbunge wa Viti Maaluma. Kutokana na ubung wake, aliteuliwa kuwa wazitika wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto na baadaye Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais- Tume ya Utumishi wa umma na Utawala Bora. Machi 2017 alifukuzwa ndani ya CCM na...